Pages

Wednesday, January 14, 2015

UWANJA WA KAITABA WAANZA KUKUKWANGULIWA TAYARI KUWEKWA NYASI BANDIA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza ukarabati katika Uwanja wa Kaitaba uliopo mkoani Kagera kuanzia Januari 12,2015.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kuwa kutokana na ukarabati huo tayari Kagera Sugar imeshaomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa ajili ya mechi zake za nyumbani. Katika hatua nyingine, Malinzi alisema kutokana na kikao cha Kamati ya Utendaji cha FIFA kilichokutana hivi karibuni kiliweka wazi kila Mwanachama wa FIFA ataendelea kupata dola za kimalekani 600,000 kwa mwaka kwa ajili ya maendeleo ya Soka. 
Muonekano wa Uwanja wa mpira wa Kaitaba Stadium wa Bukoba baada ya kuanza ukarabati huo.
Ukarabati huu wa Uwanja wa Kaitaba umeifanya mechi ya Kagera Sugar na Mbeya City kuhamishiwa kwenye Jiji la Mwanza na utachezwa siku ya Jumamosi tarehe 17.01.2015 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa mujibu wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera,watakutana na uongozi wa klabu ya Kagera Sugar ili kufahamu watatumia uwanja upi kwenye mechi zao za nyumbani za Ligi Kuu.
Kagera italazimika kuhamisha na kucheza nje ya mkoa huo mechi zake zote za Ligi Kuu hadi hapo uwanja huo wa Kaitaba utakapokamilika .

TFF tayari ilishatangaza kuwa mechi kati ya Kagera na Mbeya City,itachezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza,uwanja ambao ni mzuri na uko jirani na Mkoa wa Kagera. 
Kuhamishiwa kwa mechi za Ligi Kuu kwenye uwanja wa CCM Kirumba ni faraja kwa wapenzi,washabiki na wadau wa soka hapa,baada ya kuikosa kwa muda mrefu,tangu Toto ishuke daraja msumu uliopita. Kaitaba ni miongoni mwa viwanja ambayo vimekuwa vilalamikiwa kutokana na kuwa na mabonde na miinuko ,hivyo kuwekewa nyasi bandia kutaondoa malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya timu zilizokuwa zikiutumia kucheza na Kagera Sugar .
Mbali na Kaitaba,mwingine ambao uko kwenye ukarabati wa kuwekewa nyasi bandia ni uwanja mkongwe wa Nyamagana wa Jiji la Mwanza, ambao uko katika hatua za mwisho ili kuwekewa zuria la nyasi hizo.
Picha na Faustine Ruta, Bukoba

Taswira ya Uwanja wa kaitaba hii leo Jumatatu 12 januari 2015 unavyoonekana baada ya kuanza ukarabati huo.
Muonekano wa Uwanja wa mpira wa Kaitaba Stadium wa Bukoba baada ya kuanza ukarabati huo. Tayari Kagera Sugar imeshaomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa ajili ya mechi zake za nyumbani

No comments:

Post a Comment