Pages

Friday, January 16, 2015

MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA KAMPUNI YA MAGAZETI YA SERIKALI (TSN) AULA IDFA











CHAMA cha Soka Mkoa wa Ilala (IDFA) kimemteua Mwandishi wa Michezo wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali(TSN)  inayozalisha Habarileo,  Spotileo na Dailynews Rahel Pallangyo kuwa Kocha wa timu ya wanawake  Ilala.

Akizungumza na gazeti hili jana Katibu Mkuu wa IDFA Daudi Kanuti alisema Pallangyo kwa kushirikiana na makocha wengine wa Ilala watasaidiana kuinoa timu hiyo kwa ajili ya michuano ya kombe la taifa ya wanawake inayoendelea.

Alisema wamemteua Pallangyo kwa ajili ya mashindano hayo ya taifa ambaye ana leseni C ya ukocha ili kufanyia kazi cheti chake.
“Tunaamini tukiwapa nafasi makocha wanawake wataonyesha uwezo, na kwa vile tayari ana leseni tumempa nafasi kuifanyia kazi, asiwe kabatini kiendelee kuharibika,”alisema.
Kwa upande wa Pallangyo alisema anafurahi kupata fursa hiyo na anaahidi kuonyesha uwezo wake kwa vitendo.

“Naahidi kutumia taaluma yangu kuonyesha watu kwamba hata makocha wanawake wakipewa nafasi wanaweza kufanya mambo makubwa ili kuondoa dhana kwa jamii kuwa wanaume pekee ndio wanaoweza,”alisema 

Mtihani wa kwanza kwa Pallangyo itakuwa katika mchezo wa kwanza wa robo fainali utakaochezwa kesho jioni kati ya Ilala dhidi ya Mtwara utakaochezwa Karume.

Ilala, Kindoni na Temeke ziliingia moja kwa moja kwenye raundi ya pili ya fainali hizo

No comments:

Post a Comment