Pages

Monday, January 26, 2015

TIMU YA KOLONI YAIBUKA BINGWA WA KUWANIA KOMBE LA MH. AMOS MAKALLA.

Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, Mh Amos Makalla akiikagua timu ya Koloni kabla ya mchezo wa fainali wa kombe la Makalla jimboni humo.
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa jimbo la Mvomero, Mh Amos Makalla ( wa pili kushoto ) akiwa na Yahaya Abdalah ambaye ni mwenyekiti bodi ya ligi na meneja wa kiwanda cha Mtibwa wakifurahia wakati wa mchezo wa fainali kuwania kombe la Makalla.

Mbunge wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji,nMh Amos Makalla akikagua timu ya Mkuyuni ya Mlali.
Mgeni rasmi Mh Amos Makalla akiongea na timu kabla ya mchezo huo. 
Mh Amos Makalla ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mvomero akikabidhi zawadi mshindi wa Tatu kwa timu ya Turiani ya Kichangani.
Zawadi kwa mshindi wa pili timu ya Mkuyuni ya Mlali.
Mgeni rasmi, Mh Amos Makalla akikabidhi kombe la Makalla Cup na fedha tasilimu shilingi milioni moja kwa timu ya Koloni ya Bwagala.
Fainali za michezo mpira wa miguu kutafuta bingwa wa wilaya ya Mvomero kwa jina la Makalla Cup zimehitimishwa jana kwa maelfu ya watazamaji kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Kialawa, Kijiji cha Bwagala ambapo ulizikutanisha katika Fainali Timu Ya Koloni ya Bwagala na timu ya Mkuyuni ya Mlali. 
Bingwa wa Makalla Cup imeibuka timu ya Koloni kwa kuifunga Mkuyuni mabao 2-1. 
Mgeni rasmi na mdhamini wa Makalla CUp alikuwa Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla ambaye katika Hotuba yake alizipongeza timu zote 124 zilizoshiriki kuanzia ngazi ya kata, tarafa na hatimaye wilaya.
Amesema lengo la michezo hiyo ya kihistoria hayajawahi kufanyika jimboni Mvomero ni kuendeleza vipaji, kuwaleta pamoja vijana bila kujali itikadi za kisiasa
Gharama za kuendesha mashindano hayo kuanzia kata kwa timu 124 toka katika vijiji, Tarafa na wilaya kwa vifaa, zawadi na uendeshaji yamemgharimu fedha shilingi milioni 15, na kwa upande wa zawadi nshindi wa kwanza amejipatia fedha shilingi milioni Moja na kombe kubwa la shilingi laki tano. 
Mshindi wa pili alipata shilingi laki Sita na kombe la shilingi laki tatu, na mshindi wa tatu amepata shilingi laki Tano na kombe la shilingi laki mbili.
Amewashukuru BOA Bank kusaidia jezi seti 8, vyombo vya habari vyote,timu zote zilizoshiriki ,chama cha mpira wa miguu mvomero viongozi ngazi zote mvomero na wananchi wa mvomero kwa ushirikiano mkubwa waliompa kwa kufanikisha mashindano hayo makubwa na ya aina yake
Amehaidi kuendeleza michezo na akiwashukuru viongozi wa Kiwanda cha Mtibwa kwa kuhudhuria na kuibua vijana ambao watawasajili kwenye timu yao ya Mtibwa sugar.

No comments:

Post a Comment