Pages

Wednesday, January 7, 2015

STAND UNITED YAJIGAMBA KUIFUNGA RUVU JKT





KOCHA wa Stand United ya Shinyanga, ‘Chama la Wana’ Mganda, Mathia Lule, amejigamba kuifunga JKT Ruvu kwenye mchezo utakaochezwa Jumamosi kwenye Dimba la Chamazi jijini Dar es Salaam.

Lule ambaye amewahi kuzinoa timu za KCCA, Express na timu ya Taifa ya Vijana ya Uganda U-17 amesema kikosi chake kipo vizuri na kina morali ya hali ya juu hivyo ushindi ni haki yao

“Timu ipo vizuri hata wewe mwandishi waweza ona vile wanavyofanya mazoezi, ushindi ni wetu”, alisema kocha huyo kwa Kiswahili chanye lafudhi ya Kiganda

Pia alisema usajili waliofanya dirisha dogo umefanya timu ibadilike kiuchezaji na ufundi na kuwataka wapinzani wakae mkao wa kupata kichapo kila watakapo kutana nao.

Naye kiungo mshambuliaji Haroun Chanongo aliyesajiliwa dirisha dogo akitokea Simba ameonekana kufanya vizuri kwenye mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.

Chanongo ambaye alikuwa akichezesha kwa tahadhari asiumie alifunga mabao mawili kati ya matatu kwenye mazoezi hayo hali iliyofanya wachezaji na mashabiki waliokuwepo kumpongeza.

Lule ambaye anasaidiwa na Athuman Bilal na Emanuel Massawe amesema anafurahia kazi yake kwani anapata ushirikiano toka kwa uongozi, makocha wenzake na wachezaji pia.

No comments:

Post a Comment