Pages

Wednesday, January 7, 2015

SIMBA YA ZAMALEK KUMCHANGIA CHRISTOPHER ALEX



WACHEZAJI wa zamani wa Simba wameandaa mchezo wa kirafiki wenye lengo la kumchangia mchezaji mwenzao Christopher Alex anayesumbuliwa na maradhi ya kifua kikuu.

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam Januari 14, mwaka huu, dhidi ya veteran wa Yanga na kiingilio kitakuwa 2000.

Akizungumza jijini mchezaji wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa amewaomba mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi ili kumchangingia mchezaji huyo ambayo ni miongoni wachezaji walioifunga Zamalek 2003.

“Ninawaomba mashabiki waje kwa wingi ili kumchangia mchezaji mwenzetu apate pesa ya matibabu na kujikimu kuliko kujitokeza kumchangia wakati akiwa amekufa kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeonyesha kuwa michezo kweli ni undugu”, alisema Pawasa.

Naye Juma Kaseja ambaye akiwa miongoni mwa wachezaji waliokuwepo kwenye kikosi hicho maarufu kama Simba ya Zamalek amewaomba wote waungane kumchangia mwenzao kwani, maradhi au matatizo yameumbwa kwa ajili ya wanadamu hivyo kusitiriana ni muhimu.

Christopher Alex anasumbuliwa na maradhi ya kifua kikuu ambayo yanafanya afya yake kudhoofika, hivi sasa yupo nyumbani kwao Dodoma.

No comments:

Post a Comment