Pages

Thursday, January 8, 2015

JERRY MURO AZUNGUMZIA KASEJA NA YANGA

Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano ya Yanga Sc, Jerry Murro amezungumzia kinagaubaga juu ya mustakhabali wa goli kipa Juma Kaseja baada ya mashabiki na wapenzi wa soka kutaka kufahamu kinachoendelea kati yake na uongozi wa timu hiyo.

Akichezesha taya na Clouds Tv michezo, Muro amesema kuwa matatizo ya Kaseja na klabu ya Yanga yalianza kujionyesha baada ya yeye mwenyewe kuona hapewi kipaumbele sana kwenye klabu iyo kutokana na kukalishwa benchi tofauti na zamani alipokuwa akichejulikana kama golikipa nambari moja.

”Matatizo ya Juma Kaseja na klabu ya Yanga yalianza kujionyesha pale ambapo yeye mwenyewe Juma aliona hana kipaumbele sana kwenye klabu ya Yanga, na hii ni kutokana na yeye kutokutumiwa kwenye michezo mingi tuliyokuwa tukiicheza sisi tofauti na zamani ambavyo watu walikuwa wakimuelewa Juma Kaseja ndio golikipa nambari moja Tanzania”, alisema Muro.

Aliongeza :”lakini kwa mabadiliko ambayo Klabu ilikuwa ikiyapitia nyakati kwa nyakati na kwa mahitaji ya timu kwa wakati huu tulionao, yapo mabadiliko yamefanyika na yapo maboresho yamefanyika, mabadiliko ambayo kwa kiasi kimoja au kingine hakikuweza labda kumfurahisha Juma Kaseja yeye mwenyewe”.

Pia Muro ametolea ufafanuzi kuhusu suala zima la malipo na makubaliano mengine kati ya Kaseja na Yanga kufuatia golikipa huyo kuacha kushiriki katika mazoezi na timu hiyo.

”Sisi kwetu hufanyi mazoezi hulipwi, hata kama unamikataba, naomba nifafanue bila kupepesa macho, hata kama unamkataba…. safari hii hufanyi mazoezi, huna sababu ya kutofanya mazoezi, huna ripoti ya mwalimu, huna ripoti ya daktari wa timu, hatujui kuhusu mambo ya kwako kwenye familia, huji tuu kwenye mazoezi, ..hulipwi chochote na hatutalipa”, alisema Jerry Muro

No comments:

Post a Comment