Pages

Thursday, December 18, 2014

NUSU FAINALI CAPITAL ONE CUP LIVERPOOL KUPEPETANA NA CHELSEA

Mara baada ya Usiku huu kukamilika Mechi mbili za mwisho za Robo Fainali ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, ilifanyika Droo ya Mechi za Nusu Fainali na kushusha Bigi Mechi kati ya Liverpool na Chelsea.
Nusu Fainali nyingine itakuwa kati ya Tottenham na Sheffield United.
Mechi za Nusu Fainali zitachezwa kwa mikondo miwili ya Nyumbani na Ugenini kwenye Wiki inayoanzia Januari 19 na Marudiano yakiwa Wiki moja baadae.
Mapema Usiku huu wa Jumatano kabla Droo hii ya Nusu Fainali, Liverpool, wakicheza Ugenini kwa Vinara wa Timu ya Daraja la chini la ChampionshipBournemouth, walishinda Bao 3-1 kwa Bao 2 za Raheem Sterling na moja la Lazar Markovic wakati Wenyeji hao walipata Bao lao pekee kupitia Dan Gosling.

Kwenye Mechi nyingine ya Robo Fainali iliyochezwa pia Usiku huu huko White Hart Lane, Tottenham waliitandika Newcastle Bao 4-0 kwa Bao za Bentaleb, Chadli, Kane na Soldado.


NUSU FAINALI
"Mechi za Kwanza – Wiki ya 19 Januari 2015
"Mechi za Marudiano - Wiki ya 26 Januari 2015

FAINALI
"Jumapili 1 Machi 2015

No comments:

Post a Comment