Pages

Friday, December 19, 2014

MARIO BALOTELLI AFUNGIWA MECHI 1 NA FAINI YA £25,000

Straika wa Liverpool Mario Balotelli amefungiwa na FA, Chama cha Soka England, Mechi moja na kupigwa Faini Pauni 25,000 kwa kuposti kwenye Mtandao wa Instagram maneno ambayo baadhi yao yametuhumiwa kuwa ni ya Kibaguzi.
Mapema Mwezi huu, Balotelli alitoa Posti kwenye Instagram ikiwa na Karagosi wa Mchezo wa Kompyuta ‘Super Mario’ na kuandika maneno ambayo baadhi yao yametuhumiwa kuwa ni ya Kibaguzi.
Super Mario pia ni Jina la utani la Mario Balotelli anaesifika kwa utukutu.
Mara baada ya shutuma dhidi yake kuanza, Balotelli aliifuta Posti hiyo kwenye Instagram na pia kujibu shutuma hizo kwenye Mtandao wa Twitter na kusema: ‘Mama yangu ni Myahudi kwa hiyo wote nyamazeni tafadhali!’


BALOTELLI-ALICHOPOSTI INSTAGRAM:
-PICHA ya Karagosi wa Mchezo wa Nintendo Super Mario yenye Kichwa ‘USIWE MBAGUZI!’
-Ujumbe wa Posti hiyo:
‘Kuwa kama Mario, ni Fundi Bomba wa Kiitalia, aliebuniwa na Watu wa Japan, anaeongea Kiingereza na ana Sharubu kama Mmexico. Anaruka kama Mtu Mweusi na kunyang’anya Fedha kama Myahudi!’

Licha ya pia kuomba radhi na pia kudai Posti yake ya kwenye Twitter ni kuonyesha yeye ni mpinga Ubaguzi huku akitania, Balotelli huenda akalivaa rungu la FA baada ya kutakiwa kutoa maelezo yake kabla Saa 3 Usiku wa Ijumaa.

Balotelli alikiri kosa lake kwa FA lakini amepewa Adhabu ya Kifungo na Faini na pia kutakiwa kuhudhuria Mafunzo maalum.

No comments:

Post a Comment