Bao za Chelsea kwenye Mechi hii ambayo Derby walibaki Mtu 10 baada ya Jake Buxton kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 78 zilifungwa na Eden Hazard, Dakika ya 23, Filipe Kuis, 56, na Andre Schurrle, 82.
Bao la Derby lilifungwa na Craig Bryson Dakika ya 71.
Difenda wa Chelsea Zouma aliumia baada ya kukutana na kiwiko cha mkono wa Kipa wake Cech.
Kwenye Mechi nyingine ya Robo Fainali zilizokuwa zinapigwa kwa wakati mmoja Sheffield United, inayocheza Daraja la Ligi 1 likiwa ni Daraja la chini ya Championship, iliifunga Timu ya Ligi Kuu England, Southampton Bao 1-0.
Bao la ushindi la Sheffield lilifungwa na McNulty Dakika ya 63 na Southampton kubaki Mtu 10 baada ya Gardos kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 90.
Leo Usiku zitachezwa Robo Fainali nyingine mbili ambapo Liverpool watakuwa Wageni wa Bournemouth ambao ndio Vinara wa Daraja la Championship na Mechi nyingine ni ile pekee ya Timu za Ligi Kuu England itakayochezwa White Hart Lane Jijini London kati ya Tottenham Hotspur na Newcastle United.
Derby County vs Chelsea
No comments:
Post a Comment