Bao la pili lilifungwa tena na Danny Welbeck katika dakika ya 30 na Alexis Sánchez akamalizia la tatu na kufanya 3-0 katika dakika ya 41 baada ya kutanguliwa pasi Mesut Özil.
Kipindi cha pili dakika ya 52 Danny Welbeck alitupia hat-trick kwa kufunga bao tatu na kutimiza bao 4-0 dhidi ya Galatasaray baada ya kupata ushirikiano wa pasi ya kutanguliziwa na Alex Oxlade-Chamberlain.
Dakika ya 60 Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny anatolewa kwa kadi nyekundu na Gala kupata mkwaju wa penati.
Dakika ya 63 Burak Yılmaz alifunga mkwaju huo na kufanya 4-1. Kipa wa Arsenal D. Ospina aliyeingia kuziba nafasi ya Wojciech Szczesny alifungwa penati hiyo na ilibidi Arsenal wamtoe Alexis Sanchez ili kipa huyo aweze kuingi.
Per Mertesacker, Mesut Ozil na Lukas Podolski kwenye mazoezi
Kieran Gibbs akiwa karibu na Danny Welbeck pamoja na Ozil kabla ya kukutana na Galatasaray usiku huu kwenye Klabu Bingwa Ulaya(Uefa Champions)
No comments:
Post a Comment