Kipindi cha pili dakika ya 82 Yaya Touré aliwachoma bao la kwanza Aston Villa baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Fernando na kukatiza ndani ya box na kufunga bao hilo ambalo ndio lilianza kuwafungulia lango la magoli. Bao la pili lilifungwa dakika ya 88 na Sergio Agüero baada ya James Milner kumlisha mpira na kuachia shuti kali lililomzidi kipa wa Aston Villa ambaye alikuwa amehimili vishindo vya City vya tangu kipindi cha kwanza.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kolarov, Kompany, Mangala, Milner, Fernandinho, Touré, Silva, Džeko, Agüero
Aston Villa: Guzan, Hutton, Senderos, Baker, Cissokho, Delph, Westwood, Cleverley, Richardson, N’Zogbia, Agbonlahor.
No comments:
Post a Comment