Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha mafunzo ya usajili kwa klabu za
Ligi Daraja la Pili (SDL) yatakayofanyika kesho na keshokutwa (Oktoba 6 na 7
mwaka huu) kwenye hosteli ya TFF iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kuanzia
saa 3 asubuhi.
Mafunzo
hayo yatahusu usajili wa mtandao ambao ndiyo klabu hizo zitautumia kwa ajili ya
Ligi hiyo itakayoanza baadaye mwezi ujao katika makundi manne ya timu sita sita
kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Kesho
mafunzo hayo yatakuwa kwa ajili ya maofisa wa usajili wa klabu za Abajalo,
Arusha FC, Kiluvya United, Magereza Iringa, Milambo SC, Mji Mkuu (CDA), Mkamba
Rangers, Mshikamano, Mvuvumwa FC, Navy, Njombe Mji, Singida United, Transit
Camp, Volcano FC na Wenda FC.
Oktoba
7 mwaka huu mafunzo hayo yatahusisha maofisa usajili wa klabu za Bulyanhulu FC,
Eleven Stars, JKT Rwamkoma, Kariakoo Lindi, Mbao FC, Mpanda United, Pamba, Town
Small Boys na Ujenzi Rukwa.
No comments:
Post a Comment