Pages

Wednesday, September 10, 2014

Orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi katika ligi kuu ya soka Italia Seria yatolewa Teves nyuma ya De Rossi


De Rossi kinara kwa malipo ya pauni 77,000
Nyota wa Juventus Paul Pogba (kulia) anapata chini ya kiwango cha juu cha mshahara wa juu katika Seria A

Wachezaji wanaolipwa fedha nyingi nchini Italia katika Serie A wamewekwa bayana na mishahara hiyo imewashangaza baadhi ya watu.
Mmoja wa wachezaji wenye vipaji Paul Pogba, anapokea kiasi cha pauni £23,000 kwa wiki kwa mabingwa wa Italia Juventus wakapo ambapo kiasi cha juu kabisa cha ulipwaji wa mishahara kikiwa ni £77,000 akiwa ni kiungo wa Roma Daniele de Rossi.
Viwango hivyo vya mishahara vilivyotajwa kupitia gazeti maarufu la 'Gazetta dello Sport' pia vimeonyesha kuwa kiwango cha fedha za jumla za mishahara kimeshuka kwa mara nyingine.
Nyota wa Napoli Gonzalo Higuain na mshambuliaji wa zamani katika ligi kuu ya England (Premier League) Carlos Tevez ameungana na De Rossi katika orodha ya wachezaji watatu wa juu kimshahara huku Ashley Cole aliyejiunga na Roma akitokea katika klabu ya Chelsea msimu wa kiangazi amekatwa mshahara wake kwa kiasi kikubwa katika Serie A baada ya kukubali mshahara wa pauni £35,000 kwa wiki.
Mchezaji mwingine ambaye ameshuka kwa malipo kiangazi hii ni mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Fernando Torres, ambaye atakuwa akipokea pauni £61,000 kwa wiki katika klabu ya AC Milan ikiwa ni kiwango kilicho poromoka kwa kiwango kikubwa kutoka katika malipo ya pauni £175,000 kwa wiki alipokuwa huko London ya kaskazini.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji wanao lipwa zaidi katika ligi kuu ya nchini Italia Serie A
Juventus – Tevez £3.6m
Roma – De Rossi £5.2m
Milan – Torres and Mexes £3.2m
Inter – Vidic and Palacio £2.6m
Napoli – Higuain £4.4m
Fiorentina – Gomez £3.4m
Lazio – Klose £1.6m
Palermo – Sorrentino £0.7m
Sampdoria – Romero £1.4m
Sassuolo – Berardi £0.9m
Genoa – Matri £0.8m
Torino – Quagliarella £0.6m
Udinese – Di Natale £1m
Atalanta – Denis £0.9m
Parma – Cassano £1.2m
Verona – Toni £0.8m
Chievo – Paloschi £5.6m
Cagliari – Conti £0.4m
Cesena – Marilungo £0.3m
Empoli – Tavano £0.2m

No comments:

Post a Comment