Pages

Wednesday, September 10, 2014

Danny Welbeck awahuzunisha mashabiki wa Arsenal


Welbeck aliyejiunga na Arsenal alifunga goli mbili kwa England dhidi ya Switzerland jumatatu usiku akiwa katika kiwano cha juu
KIkosi cha timu ya taifa ya England kimetua nchini England hii leo mchana baada ya mchezo wao wa ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Switzerland ukiwa ni mchezo wa kampeni ya kuelekea kwenye michuano ya Euro 2016.
Wakati timu hiyo ikitua nchini humo mshambuliaji mpya wa Arsenal Danny Welbeck alionekana akiwa na tabasamu lakini mashabiki wa washika mitutu walionekana kuhuzunishwa na mshambuliaji huyo kuonekana akiendelea kutumia nembo ya klabu yake ya zamani ya Manchester United ikiwemo kubeba kijibegi cha mkononi kilichokuwa na picha na nembo za mashetani wekundu.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alisaini kwa washika mitutu kwa uhamisho uliogharimu pauni milioni £16 katika siku ya mwisho ya uhamisho wa kiangazi lakini inavyoonekana bado hajakabidhiwa vifaa vya matumizi vya Arsenal.
Once a red: Danny Welbeck (left) leaves the place still clutching onto his Manchester United washbag as he shares a joke with Phil Jones
Bado kuna rangi nyekundu: Danny Welbeck (kushoto) akishuka kwenye ndege akiwa bado na kimkoba cha mkononi cha United akitaniana na Phil Jones
Still got it: Welbeck holds the same United washbag during his time with the Red Devils last season
Mpaka tai bado anatumia ya mashetani wekundu
Gunners: Arsenal fans will be hoping their new signing will soon be carrying something similar to this Gunners sports bag

No comments:

Post a Comment