Pages

Wednesday, September 10, 2014

Licha ya kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya vilabu Ulaya Manchester United wavuna faida kupitia jezi


Wazee wa fedha: Makamu mwenyekiti wa United Edward Woodward (katikati), Joel Glazer (kushoto) na Richard Arnold (kulia)
Manchester United inatarajia kutangaza mapato yake ya mwaka hapo kesho ambao kiasi cha pauni milioni £420 kitatangazwa ikiwa ni mapato yenye faida ya pauni milioni £25 ambayo yametokana na uchapishaji wa jezi nakala milioni .
Mapato hayo ya mwaka yamejumuisha malipo ya meneja wa zamani David Moyes na timu yake ya makocha, lakini kiasi hicho haki akisi hasara iliyotakana na kushindwa kutinga katika michuano ya Ulaya msimu huu.
Tayari matokeo ya msingi yalikwisha kutolewa tangu mwezi Agosti katika soko la hisa la jijini New York(New York Stock Exchange).
Kitabu cha taarifa kilichoandaliwa(Prospectus) kinaeleza kuwa mapato ya jumla yanatarajiwa kuwa pauni milioni £429 mpaka pauni £434 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 mpaka 19. Ikilinganishwa na Real Madrid iliyokuwa na pauni milioni £480 lakini Real wakijumuisha mauzo ya wachezaji.
Faida kwa mwaka inatarajiwa kuwa pauni milioni £23 mpaka milioni £25 ikiwa ni chini anguko la pauni milioni £146.4 kwa mwaka 2012-13 lakini lakini ikiwa ni baada ya kodi.

No comments:

Post a Comment