Pages

Wednesday, September 10, 2014

ARSENAL KWENYE KIBARUA KIGUMU, RATIBA IMEWABANA, MECHI 7 ZIJAZO KUAMUA

Arsenal, ambao Msimu huu wamejizatiti kuwania Mataji hasa baada ya Msimu uliopita kubeba FA CUP likiwa Kombe lao la kwanza tangu 2005, wanakabiliwa na Mechi 7 mfululizo zijazo ambazo zitaamua Msimu huu kwao ni mbivu au mbichi.
Mechi hizo 7 ni za Ligi Kuu England, Kundi D la UEFA CHAMPIONS LIGI na ile ya Mtoano ya Raundi ya Tatu ya Capital One Cup.

Kwa kuanzia, Jumamosi Septemba 13, Arsenal wako kwao Emirates kuwakaribisha Mabingwa wa England Manchester City katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Siku 3 baadae Arsenal watakuwa Ugenini huko Signal Iduna Park Jijini Dortmund, Germany kuwavaa wakali Borussia Dortmund kwenye Mechi yao ya kwanza kabisa ya Kundi D la UEFA CHAMPIONS LIGI.

Kisha Siku 4 baadae wanarudi kwao England lakini Ugenini huko Villa Park kuivaa Aston Villa kweye Mechi ya Ligi na Siku 3 baadae wapo kwenye mtanange wa Mechi ya Mtoano ya Raundi ya Tatu ya Capital One Cup dhidi ya Southampton itakayochezwa Emirates.
Siku 4 baadae watacheza tena Emirates kwenye Dabi ya London ya Kaskazini dhidi ya Mahasimu wao Tottenham na hii ni Mechi ya Ligi na Siku 4 baadae Emirates tena itawaka moto kwa Mechi yao ya pili ya Kundi D la UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Galatasaray ya Uturuki.
Baada ya Siku 4 Arsenal wataenda huko Stamford Bridge kumvaa Jose Mourinho na Chelsea yake kwenye Mechi ya Ligi.
Mpaka akifikia hapo, Arsene Wenger atajitambua wazi Msimu huu wa 2014/15 amesimama wapi.

ARSENAL – Mechi 7 zijazo:
Jumamosi Septemba 13
14:45 Arsenal v Man City [Ligi Kuu England]
Jumanne Septemba 16
21:45 Borussia Dortmund v Arsenal [UEFA CHAMPIONZ LIGI - KUNDI D]
Jumamosi Septemba 20
17:00 Aston Villa v Arsenal [Ligi Kuu England]
Jumanne Septemba 23
21:45 Arsenal v Southampton [Capital One Cup – Raundi ya Tatu]
Ligi Kuu England
Jumamosi Septemba 27
19:30 Arsenal v Tottenham [Ligi Kuu England]
Jumatano Oktoba 1
21:45  Arsenal v Galatasaray [UEFA CHAMPIONS LIGI - KUNDI D]
Ligi Kuu England
Jumapili Oktoba 5
16:05 Chelsea v Arsenal [Ligi Kuu England]

No comments:

Post a Comment