Pages

Saturday, August 23, 2014

VAAN GAAL: WIKI MBILI ZILIZOPITA NILIKUWA MFALME WA MAN UTD LAKINI SASA NAONEKANA KAMA SHETANI OLD TRAFORD



Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema kipigo cha wiki iliyopita kutoka ka Swansea katika ligi kuu ya Barclays Premier hakipaswi kumgeuza yeye kuwa shetani mbele ya mashabiki wa klabu hiyo.
Mwanzo wa kazi wa Van Gaal katika klabu ya United ulikuwa mbaya wiki iliyopia na watakuwa wakielekea katika mchezo ujao Sunderland jumapili wakiwa na majeraha ambayo mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakihoji ubora wa kikosi chao kabla ya kukabiliana na Sunderland.
IKiwa tayari imefahamika kuwa mshambuliaji Danny Welbeck huenda akaondoka kikosi, presha imepanda kwa Van Gaal ndani ya Old Trafford.
Keep the faith: Louis van Gaal has called on Manchester United supporters to be patient 
Anajipa moyo: Louis van Gaal amewataka mashabiki wa Manchester United kuwa na subira
Tough time: Wayne Rooney and Co will be hoping to bounce back after their opening-day loss against Swansea
Wakati mgumu: Wayne Rooney na Co watakuwa wanatarajia kurejesha matumaini kufuatia kupoteza katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Swansea
Van Gaal amesema
'Siku zote iko namna hiyo, kwa wiki mbili zilizopita nilikuwa mfalme wa Manchester na sasa nimekuwa shetani wa Manchester.
 "Dunia ya mpira na hususani vyombo vya habari katika mpira duniani ndivyo walivyo.
'Nadhani mashabiki wa Manchester wana akili na nimekuwa nikisema katika mikutano yote ya vyombo vya habari nchini Marekani kuwa miezi mitatu ya mwanzo itakuwa migumu kwa wachezaji na mashabiki.
'Nimelisema hilo kwa mtendaji mkuu Ed Woodward na Glazers kuwa hivi ndivyo ilivyo.
'Wameniajiri mimi kwa kutokana na Filosofia yangu na si kwasababu ya uzuri wangu. 
Mimi ni mtu mzuri lakini hiyo siyo sababu ya mimi kuwepo hapa.
Making his point: Rooney will lead the line for Manchester United when they travel to Sunderland on Sunday 
Rooney atakuwa akiongoza kikosi cha Manchester United watakapo kuwa safarini Sunderland Jumapili
'Sijaajiriwa ili nifukuzwe (I’m not hired to be fired). NImeajiriwa kujenga kikosi, mchakato huo unahitaji muda, naingiza filosofia yangu katika klabu na hiyo ni ngumu kwasababu natakiwa kutoa maelezo ya kutosha.

No comments:

Post a Comment