Pages

Wednesday, August 27, 2014

TFF yamteua Bonface Wambura kuwa mkurugenzi wake wa mashindano


Mkurugenzi mpya wa TFF Bonface Wambura
SHIRIKISHO la soka nchini Tanzania TFF limemteua afisa habari wake Bonface Wambura kuwa mkurugenzi wake mpya wa mashindano ambapo atakuwa akiziba pengo la Saad Kawemba ambaye aliondolewa katika nafasi hiyo na uongozi wa Rais Jamali Malinzi siku chache baada ya uongozi wake kuingia madarakani.
Wambura ambaye kwa sifa ni mchapa kazi sasa atakuwa akisimamia mashindano mbalimbali ambayo yatakuwa chini ya TFF ikiwa ni pamoja na timu ya Taifa inapokuwa ikishiriki michuano mbalimbali ya kimataifa.
Uteuzi wa Wambura umekuja kufuatia kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi hapo jana katika ofisi za zamani za shirikisho hilo zilizopo katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume.

Katibu mkuu wa Tff Selestine mwesigwa amesema uteuzi wa Wambura utaanza kufanya kazi rasmi Septemba mosi.
Aidha Mwesigwa amesema nafasi ya afisa habari na mawasiliano itajazwa hapo baadaye na kamati ya utendaji.

No comments:

Post a Comment