Pages

Wednesday, August 27, 2014

Lukas Podolski awaaga rasmi Arsenal


Podolski aaga rasmi
Lukas Podolski ameonekana akionyesha ishara ya kumaliza utumishi wake wa soka katika klabu yake ya Arsenal kufuatia mshambuliaji huyo kutupia ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram akiwatakia kila la kheri Arsenal.
Akiwa na mafanikio ya kutwaa taji la dunia akiwa na Ujerumani nchini Brazil, mshambuliaji huyo amekuwa akifukuziwa na vilabu mbalimbali vikiwemo Juventus na kigogo cha nchini Uturuki Galatasaray.
Katika wiki za hivi karibuni wenyewe Arsenal wamekuwa katika mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo baada ya kumsajili Alexis Sanchez kutoka kwa Barcelona.

No comments:

Post a Comment