Pages

Wednesday, August 27, 2014

ANGEL Di MARIA AWEKA HISTORIA ENGLAND, ASAINI MKATABA MKATABA WA MIAKA 5 NA KLABU YA MAN UNITED

Photo: 'United are the only club I could have left Madrid for': Di Maria signs five-year deal at Old Trafford to smash British transfer recordAngel di Maria Akiwa amebeba jezi yake leo hii wakati anasaini mkataba na Klabu yake mpya ya Man United leo. Angel di Maria ametokea katika Ligi ya Spain kwenye timu ya Real Madrid.
Got him! Angel di Maria poses with Manchester United boss Louis van Gaal upon signing
Angel di Maria akiwa kwenye picha ya pamoja na Bosi wake Mpya wa  Manchester United Louis van Gaal
New motor: Di Maria poses in front of a Chevrolet car outside Aon Training Complex
Di Maria akiwa na Gari aina ya Chevrolet nje ya Uwanja wa mazoezi Aon Complex
Long-term man: Di Maria signs on a five-year deal from European champions Real Madrid
Di Maria amesaini Mkataba wa miaka 5.
MANCHESTER UNITED imetangaza rasmi kuwa Angel Di Maria amekamilisha Uhamisho wake kwa Dau la Rekodi huko Uingereza la Pauni Milioni 59.7 akitokea Real Madrid ya Spain.
Mara baada ya kukamilisha taratibu za Uhamisho, Di Maria alisema: “Nina furaha kupita kifani kujiunga na Manchester United. Nilikuwa na raha kule Spain na Klabu nyingi zilinitaka lakini Man United ndio Klabu pekee ningeweza kuiacha Real Madrid ili kujiunga nayo.
Louis van Gaal ni Kocha bora sana mwenye rekodi nzuri na nimevutiwa mno na dira na nia ya kila Mtu Klabuni hapa ili kuirudisha tena juu ambako ndiko inastahili kuwepo. Nani hamu kubwa kuanza kazi!”

Nae Meneja Louis van Gaal, akimkaribisha Di Maria, amesema: “Angel ni Kiungo wa kiwango cha Dunia lakini muhimu zaidi ni Mchezaji Kitimu. Hamna shaka kuhusu kipaji chake kisicho mfano. Ni mwepesi sana na hatari kwa Guu la Kushoto ambae anatisha Difensi yoyote ile. Uwezo wake kukokota Mpira na kuwakabili Mabeki na kuwadaa ni kitu cha furaha kukiangalia. Ni nyongeza safi sana kwa Timu!”
Chief coup: Executive vice-chairman Ed Woodward poses with Di Maria
Di Maria akimwaga wino kusaini Mkataba na Klabu ya Man United na hapa alikuwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Ed Woodward.

No comments:

Post a Comment