Pages

Thursday, August 28, 2014

AC Milan watoa nje mpando Totternham wa kubadilishana Soldado kwa Sciglio


Soldado
Tottenham imetolewa nje na AC Milan juu ya mpango wao wa badilishana mchezaji nyota Roberto Soldado na Mattia De Sciglio.
Milan walikuwa wakimfukuzia Soldado kwa lengo la kuziba pengo la Mario Balotelli ambaye amekamilisha uhamisho wake wa kuelekea Liverpool kwa pauni milioni 16 wiki hii.
Habari kutoka Italia zinaarifu kuwa Spurs walimtoa mshambuliaji huyo kwenda Milan kwa kubadilishana na De Sciglio.
Inaaminika kuwa Milan imekataa mpango huo kwasababu hawataki kumuuza mchezaji wao huyo mwenye thamani kubwa ndani ya klabu na sasa wakigeukia kwa Fernando Torres wa Chelsea.
Soldado amekuwa na wakati mgumu wa kuonyesha uwezo wa kiwango chake ndani ya ligi kuu ya Premier tangu alipojiunga na Spurs akitokea Valencia kwa fedha nyingi mwaka 2013, akifunga magoli sita tu msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment