Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 5, 2014

WORLD CUP 2014: BRAZIL 2 vs COLOMBIA 1, WENYEJI WASONGA HATUA YA ROBO FAINALI!! THIAGO SILVA NA DAVID LUIZ WAKIIFUNGIA BAO NA KUIPA USHINDI!


Bao la pili lilifungwa na David Luiz katika kipindi cha pili dakika ya 69. Kipa wa Brazil Julio César alimwangusha mchezaji wa Colombia Bacca ndani ya box na mwamuzi kudai ni penati na penati hiyo kufungwa na Mjanja Staa James Rodríguez katika dakika ya 80 na kufanya 2-1 dhidi yao. Na Mtanange kumalizika dakika 90  Brazil wakiibuka na Ushindi wa bao 2-1. Ushindi huu wa Brazil utawakutanisha na Mshindi wa wa kwanza Ugerumani siku ya Jumanne Julai 8 saa 5:00 usiku, Wao Colombia Safari imeishia hapo. Kesho Jumamosi ni Argentina vs Belgium kisha Netherlands vs Costa Rica mchezo utakaopigwa saa tano usiku huko Arena Fonte Nova, Savador Brazil.Patashika!! wakichuana kuutafuta mpiraThiago Silva akishangilia bao lakeKona ilipigwa na Neymar na Thiago Silva akaifungia bao jepesi Brazil dakika ya 7 baada ya mpira huo kuwapita walinzi wa Colombia na kufanya 1-0 dhidi ya Colombia.Kipindi cha kwanza kikiendelea...VIKOSI:
Brazil: Julio Cesar, Maicon, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Fernandinho, Paulinho, Oscar, Neymar, Hulk, Fred.
Subs: Jefferson, Dani Alves, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Bernard, Jo, Victor.

Colombia: Ospina, Zuniga, Zapata, Yepes, Armero, Guarin, Sanchez Moreno, Cuadrado, Rodriguez, Ibarbo, Gutierrez.
Subs: Vargas, Arias, Carbonero, Aguilar, Mejia, Balanta, Bacca, Ramos, Quintero, Martinez, Valdes, Mondragon.
Referee: Carlos Velasco Carballo (Spain)
Mchezaji wa Colombia James Rodriguez mapema akipasha kabla ya mtanange!
 Neymar wa Brazil akipasha
Neymar
Difenda wa Brazil  David Luiz
Taswira ya Uwanja Castelao huko Fortaleza ambao ndio unachezewa mtanange huu utaopigwa punde kati ya wenyeji Brazil vs Colombia

No comments:

Post a Comment