MSHAMBULIAJI nyota wa
timu ya taifa ya Algeria Islam Slimani amebainisha kuwa kikosi kizima
cha nchi hiyo kinatarajiwa kutoa msaada wa posho zao kwa watu wa
Gaza. Baada ya kutolewa katika hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la
Dunia na Ujerumani huku wakuonyesha kiwango bora na kuwalazimisha
wapinzani wao kwenda katika muda wa nyongeza kabla ya kufungwa mabao
2-1. Timu ilirejea nyumbani wakiwa mashujaa na wachezaji wameamua kutoa
posho zao kwa wale ambao wanazihitaji zaidi. Hatua hiyo ya Algeria
imekuja huku wawakilishi wengine wa Afrika katika michuano hiyo kama
Ghana, Nigeria na Cameroon kukumbwa na msuguano katika kambi zao
kutokana na posho hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuenguliwa
mapema.
No comments:
Post a Comment