Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 5, 2014

WORLD CUP: FRANCE 0 vs GERMANY 1, MATS HUMMELS AWATUNGUA FRANCE NA KUTINGA HATUA YA NUSU FAINALI.


Mats Hammels akipongezwa na wenzie baada ya kuifungia bao katika kipindi cha kwanza.Kipa wa France Hugo hakuona ndani!!!Mlinzi  Mats Hammels ndiye aliyewakatia tiketi Ugerumani kwa kufunga bao la pekee katika dakika ya 12  baada ya Toni Kroos kupiga mpira wa Adhabu (frii kiki) na hatimae  Mats kuwafungulia bao Ujerumani kwa kichwa katika kipindi cha kwanza. Mpira huu haukuwa wa kusisimua hata kido timu zimecheza kama zimechoka!
Kipindi cha pili hakuna aliyeliona lango la mwenzie timu zimebanana licha ya kushambuliana mpaka dakika za mwisho, Sasa Ujerumani anasubiri timu itakayoshinda kati ya Brazil na Colombia usiku huu.

Mlinzi Mats Hammels akishangilia bao lake..Dalili za kwenda Nusu Fainali!!
Mashabiki wa France kimyaaaa...huzuni kibao!safi!! Tunasonga sasa!!Kwa wenzao, Mashabiki wa Ujerumani ni Sherehe tupu!Muda unayoyoma kwa Ufaransa!

Difenda wa Ufaransa Mathieu Debuchy akigonga kichwa!

Ozil na Pogba..kwenye kuutafuta!Kipa wa Ujerumani Manuel Neuer kwenye lango lake

Karim Benzema akiachia shuti kali mbele ya Jerome BoatengMlinzi wa Ujerumani Mats Hammels akimiliki mpira dhidi ya Mathieu

Benedikt na Pogba wakigombea mpiraMsaada unatakiwa!! Mathieu Valbuena kaumia!
Antoine na Kipa Hugo si raha tena...!
Wachezaji timu zote mbili wakisalimiana kati ya France vs Germany

Kipa Hugo akijituma!

Mashabiki wa Germany wakipozi kupata picha huku wakiwa wamejipanga langi za bendera yao
Timu zote mbili zikiwa zimebeba bango la Kupiga vita Ubaguzi

Mafowadi Karim Benzema na Miroslav Klose wakisalimiana
Mapema Mashabiki wa Ufaranza Bendera zilikuwa juu..

VIKOSI:
France:
Lloris, Debuchy, Varane, Sakho, Evra, Valbuena, Pogba, Cabaye, Matuidi, Griezmann, Benzema.
Subs: Ruffier, Landreau, Cabella, Giroud, Mavuba, Mangala, Sagna, Digne, Sissoko, Remy, Koscielny, Schneiderlin.
Germany: Neuer, Lahm, Hummels, Boateng, Howedes, Ozil, Kroos, Schweinsteiger, Khedira, Muller, Klose.
Subs: Zieler, Weidenfeller, Grosskreutz, Ginter, Schurrle, Podolski, Draxler, Durm, Mertesacker, Gotze, Kramer.
Goal: Hummels 13.
Referee: Nestor Pitana (Argentina)

No comments:

Post a Comment