Louis Van
Gaal (Video juu) akiwa katika siku ya kwanza ya mazoezi na wachezaji wake wa Manchester United.
Meneja
huyo mpya aliyepewa jina la utani 'Iron Tulip' alionekana akizunguka
uwanja wa mazoezi na kujumuika na wachezaji wake kwa mara ya kwanza
sambamba na mchezaji mpya aliyesajiliwa msimu wa huu wa uhamisho wa
kiangazi kwa ada ya uhamisho ya pauni £28 Ander
Herrera.
Hii leo anatarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari Old
Trafford saa tisa mchana, kabla ya hapo kesho kuelekea nchini Marekani kwa maandalizi ya kikosi kuelekea kwenye msimu mpya.
Ikiwa nchini Marekani, United itacheza dhidi ya Los
Angeles Galaxy, Roma, Inter Milan na Real Madrid, wakati ambapo mchezo wake wa kwanza kwa Van Gaal baada ya kutua Old
Trafford ukiwa wa kirafiki dhidi ya Valencia Agosti 12.
Siku
nne baadaye United itafungua msimu kwa mchezo wa kwanza wa ligi ya
Barclays Premier League uwanja wa Old Trafford dhidi ya Swansea.
No comments:
Post a Comment