Pages

Tuesday, July 8, 2014

Mlinda mlango kinda kutoka nchini Chile, Claudio Andrés Bravo Muñoz ametambulishwa Barcelona


Claudio Andrés Bravo Muñoz
Mlinda mlango kinda kutoka nchini Chile, Claudio Andrés Bravo Muñoz metambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari mara baada ya kurejea nchini Hispania akitokea nchini kwao mwishoni mwa juma lililopita.

FC Barcelona wamemtambulisha Bravo kwa waandishi wa habari mjini Barcelona baada ya kukamilisha usajili wake, akitokea  kwenye klabu ya Real Sociedad ya nchini Hispania kabla ya fainali za kombe la dunia.

Kuchelewa kutambulishwa kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 31 kulisababishwa na hatua ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Chile, ambacho kilishiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kabla ya kufungwa na Brazil katika hatua ya 16 bora.

Bravo amesajiliwa huko Camp Nou, kwa ajili ya kuchukuwa nafasi ya Victor Valdes ambaye aligoma kusaini mkataba wa kuendelea kuitumikia FC Barcelona kwa kushinikiza kutaka kuondoka na kwenda kuendeleza soka lake kwenye klabu nyingine.
Victor Valdes
Claudio Andrés Bravo Muñoz amejiunga na Fc Barcelona kwa ada ya uhamisho wa paund million 12 na amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia klabu hiyo ya Cataluña.

No comments:

Post a Comment