Claudio Andrés Bravo Muñoz |
Mlinda mlango kinda kutoka nchini Chile, Claudio Andrés Bravo
Muñoz metambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari mara baada ya kurejea nchini
Hispania akitokea nchini kwao mwishoni mwa juma lililopita.
FC Barcelona wamemtambulisha Bravo kwa waandishi wa habari
mjini Barcelona baada ya kukamilisha usajili wake, akitokea kwenye klabu ya Real Sociedad ya nchini Hispania
kabla ya fainali za kombe la dunia.
Kuchelewa kutambulishwa kwa mlinda mlango huyo mwenye umri
wa miaka 31 kulisababishwa na hatua ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa
ya Chile, ambacho kilishiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kabla ya
kufungwa na Brazil katika hatua ya 16 bora.
Bravo amesajiliwa huko Camp Nou, kwa ajili ya kuchukuwa
nafasi ya Victor Valdes ambaye aligoma kusaini mkataba wa kuendelea kuitumikia
FC Barcelona kwa kushinikiza kutaka kuondoka na kwenda kuendeleza soka lake
kwenye klabu nyingine.
Victor Valdes |
Claudio Andrés Bravo Muñoz amejiunga na Fc Barcelona kwa
ada ya uhamisho wa paund million 12 na amesaini mkataba wa miaka minne wa
kuitumikia klabu hiyo ya Cataluña.
No comments:
Post a Comment