Pages

Tuesday, July 8, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: NUSU FAINALI YA KWANZA LEO HII JUMANNE, BRAZIL v GERMANY. REFA NI MARCO RODRIQUEZ WA MEXICO



Hii itakuwa ni mara ya pili tu kwa Brazil na Germany kukutana kwenye Kombe la Dunia wakati watakapocheza Nusu Fainali huko Estadio Mineirão Mjini Belo Horizonte Nchini Brazil.
Mara pekee waliyokutana ni Mwaka 2002 kwenye Fainali ya Kombe la Dunia huko Yokohama, Japan na Brazil kushinda Bao 2-0, kwa Bao za Ronaldo, na kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya 5, hiyo ikiwa mara yao ya mwisho na wakati huo Kocha wao ni huyu huyu wa sasa Luiz Felipe Scolari.


USO KWA USO 
*Mechi 21: Brazil wameshinda Mechi 12, Germany 4, Sare 5
Mechi za hivi karibuni:  

*10 Agosti 2011: Germany 3-2 Brazil- Kirafiki, Mercedes-Benz Arena
*25 Juni 2005: Germany 2-3 Brazil- Fifa Kombe la Mabara Nusu Fainali, Frankenstadion, Nuremberg
*7 Sep 2004: Germany 1-1 Brazil- Kirafiki, Berlin
*30 Juni 2002: Brazil 2-0 Germany- 2002 Fainali Kombe la Dunia, International Stadium, Yokohama 

*24 Julai 1999: Brazil 4-0 Germany- Kombe la Mabara Makundi, Estadio Jalisco, Guadalajara


VIKOSI VINATARAJIWA KUWA HIVI:-
Brazil v Germany
Tuesday, July 8, 2014
Estadio Mineirao, Belo Horizonte
Brazil 

(Possible, 4-2-3-1): Cesar; Maicon, Luiz, Dante, Marcelo; Gustavo, Fernandinho; Willian, Oscar, Hulk; Fred.
Germany

 (Possible, 4-3-3): Neuer; Lahm, Hummels, Boateng, Höwedes; Khedira, Schweinsteiger, Kroos; Özil, Müller, Götze.
Referee: Marco Rodríguez (Mexico).

No comments:

Post a Comment