Pages

Friday, July 25, 2014

Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski kuukosa mchezo wa ufunguzi wa ligi ya England dhidi ya Crystal Palace

Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski hawatakuwepo katika mchezo wa kuanza msimu mpya 2014/15
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ametanabaisha kuwa nyota wake walicheza fainali ya kombe la dunia hawatakuwepo katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya England 'Premier League' dhidi ya Crystal Palace.
Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski wanastahili mapumziko marefu kufuatia mafanikio ya Ujerumani nchini  Brazil.
Watatu hao hawatarejea kikosini wakati huu wa maandalizi ya timu mpaka Agosti 11 ambapo itakuwa imesalia siku tano kuelekea mchezo wa kwanza dhidi ya kikosi cha kocha Tony Pulis.
Arsene Wenger poses for a picture with New York Red Bulls star Thierry Henry (second left)
Arsene Wenger akipiga picha na nyota wa New York Red Bulls ambaye pia ni nahodha wa zamani wa Arsenal  Thierry Henry (wa pili kushoto)
The Arsenal players train in the New York Red Bulls stadium ahead of Saturday's match
Wachezaji wa Arsenal wakiwa mazoezini uwanja wa New York Red Bulls kabla ya mchezo wao wa kesho wa kujipima nguvu hapo kesho
Arsene Wenger chats to former Gunners hero Thierry Henry who now plays for the New York Red Bulls
Arsene Wenger akiongea na shujaa wake wa zamani Thierry Henry ambaye sasa anachezea New York Red Bulls

Wenger  amekataa kuthibitisha kuwa amemuadabisha nyota wake Jack Wilshere ambaye alipigwa picha akivuta sigara Las Vegas lakini amedokeza kuwa shirikisho la soka duniani FIFA linapaswa kufikiria upya juu ya ratiba ya michezo yake ya kobe la dunia ambayo imetoa ugumu kwa maandalizi ya kikosi chake.A fit again Abou Diaby tussled for the ball during the session in New York
Abou Diaby anaonekana kurejea upya msimu ujao baada ya majeruhi ya msimu uliopita, pichani anaonekana akiwa mazoezini New York
Jack Wilshere tries a back flick during training in the Red Bull Arena on Thursday
Mvuta sigara aliyeshindikana Jack Wilshere akionekana kujifua mazoezini Red Bull Arena jana.
Thierry Henry joined boss Arsene Wenger on the sidelines as the Arsenal players went through their paces
Thierry Henry ameungana na bosi wake zamani Arsene Wenger pembezoni mwa wachezaji wa Arsenal wakati wa mazoezi

No comments:

Post a Comment