KOCHA
mpya Manchester United Louis van Gaal na Kikosi chake cha Wachezaji 25
wametua huko Los Angeles Marekani Alfajiri ya Leo tayari kwa Ziara yao
ya kabla Msimu mpya kuanza.
Wakiwa wamefikia Hoteli ya Beverly Hills, Louis van Gaal alikichukua Kikosi chake kuzunguka Bichi ya Santa Monica ili kunyoosha miguu baada ya safari ndefu kutoka Jiji la Manchester.
Huko Marekani, Man United watacheza Mechi 4 na ya kwanza ni Julai 23 dhidi ya LA Galaxy ya USA kuwania Chevrolet Cup.
Baada ya hiyo watapambana na AS Roma, Inter Milan na Real Madrid kuwania International Champions Cup na wakifuzu kuingia Fainali watacheza Mechi yao ya 5 huko Marekani hapo Agosti 4.
Mechi ya kwanza kwa Van Gaal Uwanja wa Nyumbani Old Trafford ni dhidi ya Valencia hapo Agosti 12 na Siku 4 baadae wataanza Msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa kuivaa Swansea City pia Uwanja wa Old Trafford.
Kikosi cha Man United kilianza Mazoezi Julai 4 chini ya Meneja Msaidizi Ryan Giggs na Makocha wapya walioletwa na Van Gaal, Albert Stuivenberg, Marcel Bout na Kocha wa Makipa Frans Hoek.
Wachezaji ambao bado hawajajiunga na Kikosi hicho baada ya kupewa muda zaidi wa Mapumziko baada kuwa huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia ni Robin van Persie, Marouane Fellaini na Javier Hernandez ‘Chicharito’.
Pia Michael Carrick na Anderson wamekosekana kwa sababu ni majeruhi huku Patrice Evra akiachwa kwa sababu ya matarajio ya Uhamisho wake kwenda Juventus.
Akizungumzia Mazoezi ya Timu yake, Van Gaal alisema kumekuwa na ugumu kutokana na Wachezaji kurudi Klabuni kwa wakati tofauti kutokana na Kombe la Dunia na hivyo wamepaswa kuwapa Mazoezi kibinafsi zaidi.
Lakini Mchezaji mpya wa Man United, Ander Herrera, amesema: “Hizi Wiki za kwanza zimekuwa safi. Mazoezi ni mazuri, sawa na Athletic Bilbao, ambako tunafanya mazoezi sana na Mpira. Makocha wanataka tumiliki Mpira na kuudhibiti na hili ni safi kwa sisi Wachezaji!”Kocha Van Gaal akiteta jambo na Wayne Rooney

No comments:
Post a Comment