Kocha ya ukocha wa mpira wa miguu
ya leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
iliyokuwa ianze jana jijini Dar es Salaam sasa itafanyika
mwezi ujao.
Marekebisho
hayo yamefanyika kutokana na maelekezo ya CAF ambayo ndiyo itakayosimamia na
kuendesha kozi hiyo itakayoshirikisha makocha wenye leseni B za shirikisho hilo.
Tarehe
rasmi ya kuanza kozi hiyo itatangazwa wiki ijayo. Mwezi uliopita Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na CAF liliendehsa kozi ya
leseni B iliyoshirikisha makocha 29 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment