Meneja
mpya wa Manchester United manager Louis van Gaal amewasili uwanja wa
mazoezi ya Manchester United Carrington hii leo kuanza kazi ya ukocha.
Mduchi
huyo alionekana kukwepa kamera za waandishi wa habari wakati akiingia
klabu hapo lakini akaonekana kupitia ukurasa rasmi wa twitter akiwa
pamoja na kocha msaidizi wake Ryan Giggs
akiwa sambamba na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward.
Kocha
mdushi Van Gaal amerejea akitokea kazini katika kombe la dunia ambako
alikuwa akiiongoza Uholanzi ambayo ilifikia hatua ya nusu ya fainali ya
kombe la dunia kabla ya kumaliza katika nafasi ya tatu baada kuichapa
Brazil
Majadiliano:Giggs, Van Gaal NA Clive Woodward.
United itakuwa ikielekea Marekani siku zijazo na Giggs ana furahia mazoezi mpaka sasa
Wakati anawasili mwezi May, Van Gaal alikaririwa akisema
'Hii klabu ina matarajio makubwa, na mimi pia nina matarajio makubwa. Kwa pamoja nina amini tutatengeneza historia.
'Kufanya kazi kama meneja katika klabu ya Manchester United, klabu kubwa duniani, kunanifanya nijisikie ni mwenye fahari'.
Louis Van Gaal akitua uwanja wa ndege wa Manchester kwa ndege binafsi mchana wa leo
United
imekuwa ikihusishwa na mpango wa kumsajili kiungo wa Juventus Arturo
Vidal, nyota wa kimataifa wa Chile, na tetezi zinazidi kuongezekana
kufuatia kuondoka kwa meneja Antonio Conte katika klabu hiyo ya Juve.
No comments:
Post a Comment