|
Jua tamuFun in the sun: Cesc Fabregas na mpenzi wake Daniella Semaan wakifurahia mapumziko yao wakiwa na binti yao Lia
|
Kiungo
wa zamani wa Arsenal alipata wasaa wa ku-enjoy mapunziko yake ya msimu
akiwa na familia yake kabla ya kujiunga na klabu yake mpya ya Chelsea
kwa maandalizi ya kuanza msimu mpya 2014/15.
Fabregas
akiwa na mpenzi wake ambaye ndie mama wa watoto wake Daniella Semaan
wakiwa na binti yao Lia walijitupa ufukweni Sardinia ufukweni wakiota
jua la pwani na hata kufurahia maji ya bahari.
Cesc
Fabregas amesaini kujiunga na Chelsea akitokea Barcelona kwa ada ya
uhamisho ya pauni milioni £30 kwa mkataba wa miaka mitano.
Wakati
yeye akifanya yake, upande mwingine, Chelsea wakianza kwa ushindi wa
mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza kabisa wa pre-season na Wycombe.
John
Terry na Branislav Ivanovic wote wakiingia kwenye kitabu cha mabao
mchezo ambao nyota wa kesho yaani wachezaji vijana Patrick Bamford na
Izzy Brown nao wakiandika mabao.
Kikosi cha kocha Jose
Mourinho kitafungua msimu mpya Agosti 16 dhidi ya timu mpya katika ligi ya Premier, Burnley
kabla ya kurejea nyumbani Stamford Bridge kwa mchezo dhidi ya timu nyingine ambayo nayo mpya katika msimu ya Leicester
City.
Wasaa wa kujiachia: Cesc na Daniella wakilitega jua wakiwa na binti yao Lia
Daniella
Semaan kushoto aliachana na mumewe aliyekuwa milionea mwaka 2011 kwa
ajili ya penzi la Cesc Fabregas, 'kupendwa ndio huku'.
No comments:
Post a Comment