Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, June 20, 2014

XABI ALONSO: ‘ZAMA ZA SPAIN ZIMEKWISHA!’ ‘TULIJUA NAMNA YA KUSHINDA, SASA INABIDI TUJUE NAMNA YA KUSHINDWA!’

Kiungo wa Spain Xabi Alonso amekiri kuwa sasa zama za Spain zimekwisha baada ya Jana kuvuliwa Ubingwa wa Dunia na kutupwa nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Jana Spain walipigwa 2-0 na Chile kwenye Mechi yao ya Pili ya Kundi B na hiki ni kipigo chao cha pili baada kudundwa 5-1 na Netherlands kwenye Mechi ya kwanza.

Spain, ambao wamebakisha Mechi 1 tu ya Kundi B ya kukamilisha Ratiba tu watakapocheza na Australia ambao nao wapo nje, wameweka Rekodi ya kuwa Bingwa wa Kwanza wa Dunia kutolewa nje ya Fainali za Kombe la Dunia baada ya Mechi 2 tu.
Alonso, ambae ni Kiungo wa Real Madrid aliewahi kuchezea Liverpool, amesema: “Vitu vinabadilika. Zama zinaisha kwa kufungwa…na hiki kilikuwa kipigo kichungu. Hatukutegemea lakini ndio mchezo. Hivi vitu vinatokea. Hatukutegemea lakini ni lazima tuyakabili majonzi yetu vile vile kama tunavyofurahia, kama Wanaume.” Spain v Chile
Alonso amekiri wameshindwa kuendeleza ‘njaa’ ya mafanikio na zama zao za ushindi kwa Rika lake la Wachezaji wa Spain sasa zimekwisha.
Spain v Chile
Amesema: “Tumecheza dhidi ya Timu zilizojitayarisha vyema na sasa tunarudi nyumbani. Inauma lakini huu ndio mpira. Kama nilivyosema, tulijua namna ya kushinda, sasa inabidi tujue namna ya kushindwa!” Spain v Chile
Nae Nahodha wa Spain, Kipa Iker Casillas, ambae alifanya makosa makubwa kwenye Mechi zote mbili walizofungwa, amesema: “Tunaomba Watu watusamehe. Sisi ndio tunaowajibika lakini pia ni wa kwanza kusikia uchungu.” Spain v Chile
Kubwagwa kwa Spain kulilifanya Gazeti kubwa la Michezo huko Spain, MARCA, liweke Bango: “NI MWISHO-NI MWISHO WA KUSIKITISHA KWA ZAMA ZA KISHUJAA ZA LA ROJA”

No comments:

Post a Comment