Pages

Thursday, April 3, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: FULL TIME- REAL MADRID 3 v BORUSSIA DORTMUND 0, GARETH BALE, ISCO NA RONALDO WAMALIZA KISASI! RONALDO AFUNGA BAO 14 MSIMU MMOJA UEFA CHAMPIONS!


Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake la tatu kwa timu yake Real dhidi ya Dortmund usiku huu.

Cristiano Ronaldo leo ameendelea kupata zaidi bao na leo hii akiwafunga bao la tatu Borussia Dortmund na kufikisha bao 14.
Real Madrid, wakicheza Uwanjan kwao Santiago Bernabeu Jijini Madrid Nchini Spain, Usiku huu wameichapa Borussia Dortmund Bao 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Gareth Bale ndie aliefunga Bao la Kwanza katika Dakika ya 3 tu baada kuunganisha pasi safi ya Daniel Carvajal na kumzidi akili Kipa Roman Weidenfeller
Bao la Pili la Real lilifungwa katika Dakika ya 27 kupitia Isco kwa Shuti la chini toka Mita 20.
Dakika ya 3 Mchezaji Gareth Bale anaipachikia bao Real Madrid baada ya kupewa pasi na Daniel Carvajal na kufanya 1-0 dhidi ya Borussia Dortmund. Dakika ya 27 kipindi cha kwanza Real wanaongeza bao na kufanya 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund, Bao likifungwa na Isco. Bao hizo mbili zimetosha mpaka mapumziko Real wakiwa mbele ya 2-0.
Kipindi cha pili dakika ya 57 C. Ronaldo anaipachikia bao la tatu na kufanya 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund baada ya kupewa pasi safi na Luka Modric.Wachezaji wa Real wakimpongeza Bale baada ya kuwapachikia bao na kuwaweka mbele ya bao 1-0 dhidi ya Borussia Dortmund.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa Real 2 Dortmund 0.
Katika Dakika ya 57, Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, alipiga Bao la 3 baada kumtoka Kipa Roman Weidenfeller kufuatia kupokea pasi safi ya Luka Modric.
Hilo ni Bao la 14 kwa Ronaldo kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu huu na ameifikia Rekodi ya Ronaldo ya Lionel Messi aliefunga Bao 14 katika Mechi 11 za UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu wa 2011/12 wakati Ronaldo amechukua Mechi 8 tu.Kocha wa Dortmund Juergen Klopp
Ronaldo hakumaliza Mechi hii baada ya kuumia na kutolewa nje katika Dakika ya 80.Cristiano Ronaldo akituliza mpira.Timu hizi zitarudiana huko Signal Iduna Park, Jijini Dortmund, Germany Jumanne Aprili 8.

No comments:

Post a Comment