TIMU ya
Taifa ya Wanawake inaondoka nchini kesho saa mbili asubuhi kwenda nchini Zambia
na ndege ya Kampuni ya Fastjet ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri.
Twiga stars inakabiliwa na mechi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Zambia ya kuwania tiketi
ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika baadaye mwaka
huu jijini Windhoek, Namibia.
Akizungumza wakati wa kuwaaga
wachezaji wa Twiga, Mgeni rasmi Katibu wa Kamati ya Olympiki Tanzania, Filbert
Bayi alisema kuwa ana imani na timu hiyo kwani ni ina wachezaji ambao wamekaa
pamoja kwa muda mrefu.
“Nakumbuka 2011 timu hii ikiwa na
baadhi ya wachezaji ninaowaonana hapa ilishiriki kwenye mashindano ya Olympiki
Afrika hivyo naamini itafanya vizuri”, alisema Bayi.
Pia Bayi alisema anampongeza kocha
Kaijage kwa kazi yake nzuri ya kufundisha na kurejesha heshima kwa Twiga kwani
wanaonekana nadhifu kama wanawake.
Naye kocha Kaijage alisema kuwa
anashukuru timu yake ipo vizuri kwani
imejiandaa vya kutosha hivyo wana uhakika watakwenda kufanya vizuri.
Naye nahodha wa timu hiyo, Sophia
Mwasikili alisema wanaamini watafanya vizuri kulingana na mafunddisho
waliyoyapata kwa kocha wao ila dua na sapoti za watanzania zinahitajika ili
wafanye vizuri zaidi.
“Sisi tupo vizuri kuhakikisha
tunashinda mchezo huo wa ugenini ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kusonga
mbele ila tunawaomba watanzania watupe sapoti na dua zao”, alisema Sophia
Twiga Stars inaondoka na kikosi cha
wachezaji 19 na benchi la ufundi lenye watu watano mechi hiyo itakayooanza saa
9 kamili kwa saa za Zambia. Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
No comments:
Post a Comment