Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 12, 2014

SIMBA WAAPA KUFUNGA MBEYA CITY SOKOINE




WACHEZAJI wa Simba SC wameahidi kwenda kupigana kufa na kupona kwa ajili ya ushindi dhidi ya Mbeya City Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Kikao cha jana baina ya wachezaji wa klabu hiyo na Mwenyekiti wao, Alhaj Ismail Aden Rage makao makuu ya klabu, kilimalizika vizuri, japokuwa kilianza vibaya

Baada ya Mwenyekiti kuhoji juu ya kufungwa na Mgambo JKT 1-0 Jumapili Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wachezaji walitoa sababu lukuki.

Miongoni mwa sababu hizo ni madai ya kucheleweshewa mishahara na pia kocha wao, Zdravko Logarusic kuwatukana sana.

Uongozi ulipangua hoja hizo vizuri na mwafaka ukafikiwa kwamba Simba SC iende Mbeya kwa nguvu moja ya kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuwafunga Mbeya City Uwanja wa Sokoine.    

Simba SC inaweza kupanda hadi nafasi ya tatu ikishinda Jumamosi, kwani itafikisha pointi 34 sawa na Mbeya City lakini yenyewe itasogea nyuma ya Yanga SC yenye pointi 35, kwa sababu ina wastani mzuri zaidi wa mabao ya kufunga na kufungwa.

No comments:

Post a Comment