Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 18, 2014

CISSOKHO: NITAFANYA KILA NALOWEZA KUHAKIKISHA NAISAIDIA LIVERPOOL

BEKI wa kushoto wa klabu ya Liverpool, Aly Cissokho anatambua kuwa sio aina ya mchezaji ambaye ni maarufu lakini ameapa kucheza kwa bidii wakati akiwa Anfield. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa, amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Liverpool toka uanze mwaka huu lakini amekuwa akishambuliwa na baadhi wachambuzi wa mambo ya soka akiwemo Michael Owen kwa jinsi anavyomiliki mpira na anavyoshambulia.
Na wakati akikiri kuwa hawezi kumridhisha kila mtu, amepania kuonyesha thamani yake mpaka mwishoni mwa msimu wakati uamuzi utakapotolewa kama anaweza kupata mkataba wa kudumu kutoka Valencia. Cissokho amesema malengo yake ni kujituma kadri anavyoweza kwa ajili ya Liverpool na kufurahia kila dakika halafu itajulikana huko mbele itakavyokuwa. Beki huyo alicheza mechi yake ya kwanza toka achukuliwe kwa mkopo kutoka Valencia Agosti 24 katika mchezo wa ligi dhidi ya Aston Villa lakini siku tatu baadae alipata majeruhi yaliyomfanya akae nje ya uwanja kwa wiki sita.Cissokho akionesha kiwango moja ya mechi Liverpool walipocheza na Newcastle.Aly Cissokho, Daniel Sturridge (katikati) waLiverpool wakipongezana pamoja na Luis Suarez

No comments:

Post a Comment