Pages

Saturday, January 4, 2014

TEMEKE QUEENS YATWAA KOMBE LA TAIFA CUP LEO BAADA YA KUIFUNGA MOROGORO QUEENS



TIMU ya mchezo wa pete ya mkoa wa Temeke imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa mashindano ya Taifa Cup, baada ya kuifungaMorogoro mabao 52-38 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Temeke walianza kuliandama lango la Morogoro  tangu robo ya kwanza ya mchezo kwani walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 15 na Morogoro  wakiwa na mabao 7 pia Temeke walizidi kung’aa kwenye robo ya pili baada ya kuifunga Morogoro  mabao 12 kwa 8.

Kwenye robo ya tatu Morogoro  walizidi kupotea  na kujikuta wakifungwa mabao 14 kwa 10 na robo ya nne ya kukamilisha mchezo Morogoro walizinduka na kuifunga Temeke mabao 17  kwa 14. 

Morogoro hawatamsahau GS wa Temeke Mwanaidi Hassan kwani ndiye alikuwa mwiba mchungu kwa kutumbukiza mabao mengi  katika mchezo wao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu alisema kuwa Temeke wanafanya vizuri na watatetea ubingwa wake kutokana na maandalizi mazuri walioyafanya 

Naye Mwenyekiti  wa Chama cha Netbali (CHANETA) Anna Kibira alimpongeza na wafadhili waliojitoa kukisaidia Chama chake na kuomba wadau wengine kujitokeza kuisaidia timu ya Taifa “Kilimanjaro Queens” inayokwenda kwenye mashindano ya Mapainduzi.















No comments:

Post a Comment