Pages

Saturday, January 4, 2014

MANCHESTER CITY YATOKA SARE NA BLACKBURN 1-1, FA CUP LEO

Alvaro Negredo akishangilia bao lake katika dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza.Ni kama raha iliyokuwa ikisubiriwa muda wote! Wachezaji wa City wakishangilia bao lao mbele ya mashabiki wao kiduchu kwenye uwanja wa Ewhood Park mwishoni mwa kipindi cha kwanza.Mchezaji wa City Edin Dzeko akijaribu kuwatoka mabeki wa Blackburn.
Bao la City limefungwa dakika ya mwishoni kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wao Negredo baada ya kupigwa mpira wa kona na hatimaye Negredo kuupata ukiwa umepoa na kuunganisha hadi langoni. City wameeenda mapumziko kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Blackburn Rovers. Kipindi cha pili dakika ya 55 Kona iliyopigwa na mchezaji wa Blackburn kujitwisha kichwa na hatimae kipa wa City Pantilimon kuutema na kisha Danny kumalizia mpira huo na kufanya matange matokeo yawe sare ya 1-1.
Scott Dann akisawazisha na kufanya 1-1 Ushangilia wa aina yake kwa kubebwa baada ya kusawazisha!
Shuti la Ben Marhsall  likizuiliwa na Joleon Lescott wa CityMchezaji wa City City David Silva na Ben Marshall wa Blackburn wakigombea mpira hapa kipindi cha kwanza
Kocha wa   Blackburn Rovers Gary Bowyer
Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini akiwa kakaa kwenye benchi kwenye uwanja wa Ewood Park Chris Taylor kwenye patashika na  Gael Clichy Mchezaji wa Blackburn Jason Lowe na wa Manchester City Alvaro Negredo wakisubiri mpira hapa huku wote wakiukodolea macho!
VIKOSI:
Blackburn Rovers: Robinson, Henley, Dann, Hanley, Spurr, Williamson (King 64), Lowe, Taylor, Cairney, Marshall (Campbell 80), Gestede (Rhodes 80)
Substitutes: Eastwood, Kilgallon, Rochina, Judge
Scorer: Dann 54
Manchester City: Pantilimon; Boyata, Lescott, Nastasic, Clichy; Fernandinho (Yaya Toure 64), Garcia; Milner, Silva (Zabaleta 88); Negredo (Jesus Navas 75), Dzeko

Substitutes: Hart, Kompany, Kolarov, Lopes
Scorer: Negredo 44
Referee: Michael Oliver

No comments:

Post a Comment