Pages

Wednesday, January 1, 2014

TANZANIA STARS YAFUNGWA NA A.S KOTOKO YA BURUNDI

Benchi la Tanzania Stars

Benchi la A.S Kotoko





TIMU ya wachezaji wa zamani ‘Tanzania Stars’ leo imeonja kipigo cha mabao 4-3 toka kwa A.S Kotoko FC ya Burundi katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Tanzania Stars ilijikuta ikionja dhahama hiyo toka kwa wageni wao katika kipindi cha kwanza na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa wamefungwa mabao 4-0.

Mabao ya A.S Kotoko yalifungwa na Nzeimana Jimmy aliyefunga mabao mawili, Said Mtoka na Amuri Salum aliyeshindilia msumari wa mwisho.

Kipindi cha pili Tanzania stars walibadilika na kutandaza kabumbu safi ambalo liliwavutia mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo na kufanikiwa kupata bao la kufuta machozi kupitia kwa Zuberi Katwila.

Wakiendelea kutumia uzoefu wao Tanzania stars walipata mabao mengine mawili kupitia kwa Dotto Peter kwa njia ya penati na kufanya mchezo kumalizika kwa mabao 4-3.

Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha wa Tanzania Stars, Mohamed Hussein “Mmachinga’ alisema kuwa kipigo walichokipata kinatokana na wachezaji wengi kuchelewa kufika lakini akawasifu wapinzani wao kuwa ni wazuri na wana mbio.

“Kufungwa ni sehemu ya mchezo ila kipigo kimetokana na wachezaji kuchelewa  kufika hivyo kuanza wakiwa pungufu ila hata hivyo wapinzani wetu ni wazuri na wana kasi sana wanapopata mpira”, alisema Hussein.


No comments:

Post a Comment