Pages

Thursday, January 2, 2014

ASHANTI YAFUNGWA NA TUSKER MAPINDUZI CUP

ASHANTI United imeanza vibaya michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kufungwa bao 1-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa Kundi C jana usiku, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bao pekee lililoizamisha Ashanti lilifungwa na Joshua Oyoo dakika ya 24, akiunganisha krosi ya Ali Abondo.
Kocha Kibadeni kushoto na wasaidizi wake, Nico Kiondo na Mfaume Athumani katika mechi ya leo Uwanja wa Amaan

Kocha mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ alibadilisha wachezaji wanne kwa mpigo mwanzoni mwa kipindi cha pili, ili kuongeza uhai katika timu yake.
Aliwatoa Anthony Matangalu, Juma Jabu, Faki Hakika na Joseph Mahundi na kuwaingiza Hussein Mkongo, Abdul Mtiro, Paul Maona na Malick Jaffar.
Pamoja na mabadiliko hayo, Ashanti iliyochukua nafasi ya Yanga SC iliyojitoa  kwenye mashindano haya, haikuweza kupata bao la kusawazisha.

Mshambuliaji wa Ashanti United, Ekeye Breyton Obina akienda chini baada ya kupitiwa na beki wa Tusker FC ya Kenya katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mapinduzi, usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Tusker ilishinda 1-0. Pamoja na kufungwa, Ashanti iliyochukua nafasi ya Yanga iliyojitoa, imeonyesha ni timu ya ushindani
Kipa wa Tusker, Samuel Odhambo akiokoa hatari langoni mwake dhidi ya mshambuliaji wa Ashanti
Mshambuliaji wa Ashanti United, Kassim Kilungo kushoto akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Tusker kulia
Mchezaji wa Tusker akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Ashanti,
Wachezaji wa Tusker kulia na wa Ashanti kushoto wakigombea mpira wa juu
Samuel Odhiambo aliinyima mabao Ashanti leo
Kiungo wa Ashanti, Malik Jaffar akiambaa kulia
Kikosi cha Ashanti
Kwa hisani ya Bin Zubeiry

No comments:

Post a Comment