Pages

Wednesday, January 1, 2014

WAAMUZI WA ILALA WAWAFUNDISHA SOKA WAAMUZI WA KINONDONI KWA KUWABUGIZA 3-0

Mshambuliaji wa Ilala, Omar Miyala akikimbia na mpira huko beki wa  Kinondoni Omari Mfaume (katikati) akimkimbiza wakati wa mchezo uliochezwa Uwanja wa Karume leo




 
Viongozi wa Soka mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia mpambano

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa CCM, Ilala akisalimiana na wachezaji wa Ilala

Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa Kinondoni

Kikosi cha Kinondoni



Kikosi cha Ilala



TIMU ya Waamuzi wa Ilala leo waliifunga timu ya waamuzi wa Kinondoni mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao ulijaa kila aina ya burudani ulishuhudia Ilala wakienda mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Kaniki Miraji akiunganisha pasi ya Emanuel Kazimoto.

Bao la pili lilifungwa na Said Ndege kwa njia ya penati baada ya beki wa Kinondoni kumwangusha Innocent Mwakitamila katika eneo la goli.
Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko yaliyosababisha upinzani kuwa mkali kwani Kinondoni walipata penati mara mbili lakini washambuliaji wake Hashim Abdallah na Wema Ngotwa walipiga nje.

Wakati Kinondoni wakikosa penati hizo Ilala nao walikosa penati moja iliyopigwa na Emanuel Kazimoto ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo.
Ilala walipata bao la tatu kupitia kwa mshambuliaji mkongwe Seif Kihange aliyeunganisha krosi ya Omari Miyala.

Akizungumza baada ya mchezo huo Mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Ilala, Asaa Simba aliwashukuru waamuzi kwa mchezo mzuri walionesha kwani inadhihirisha kuwa si kuchezesha tu bali pia wanajua kucheza.

“Nashukuru mmetupa burudani ya mwaka mpya pia mmedhihirisha kuwa siyo kuchezesha wengine tu mnajua hata kucheza na nyie mnafahamu”, alisema.

Pia walikuwepo viongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Viongozi wa chama cha soka Ilala na viongozi wwa vyama vya waamuzi mkoa, na wilaya za mkoa wa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment