Pages

Monday, January 27, 2014

STAN BINGWA MPYA WA AUSTARALIA OPEN

Stanislas Wawrinka raia wa Uswis amefanikiwa kutwaa taji la michuano ya wazi ya Australia kwa kumchapa Mhispania Rafael Nadal katika mchezo wa fainali.

Wawrinka alimfunga Nadal aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya mgongo kwa seti tatu kwa moja, ikiwa ni kwa matokeo ya 6-3 6-2 3-6 6-3.
Anakuwa raia wa pili wa Uswis kunyakuwa taji la Grand Slam kwa upande wa wanaume kwa mchezo wa tenesi wa mchezaji mmoja mmoja.
Pia ni mtu wa pili kunyakuwa taji kubwa kama hilo akiwa ametoka nje ya vinara wanne wa juu wa dunia wa mchezo wa tenesi, baada ya Juan Martin Del Potro kufanya hivyo kwenye michuano ya US Open mwaka 2009.
Nadal ambaye awali alisema kusumbuliwa na matatizo ya mgongo lakini hakujitoa kwenye michuano hiyo ambayo imefikia tamati huko Melbourne Park.
" Sikupenda kusema kwamba sitocheza mchezo wa fainali, ni jambo ambalo nachukia sana hata kama niligundua kuwa nina maumivu ya majeraha" Alisema Nadala mwenye umri wa miaka 27.
" Huu sio wakati wa kuzungumzia maumivu niliyoyapata, ila ni wakati wa kumpongeza Stan. Amecheza vizuri sana na ukweli anastahili taji hili.
Ni mtu mwema, mtu mzuri na rafiki yangu, nina furaha sana kwake kuwa bingwa" Alisema Nadal.
Naye Wawrinka alimsifu Nadal kwa kuwa bingwa wa kweli na kinara wa kweli wa tenesi duniani kwa wanaume, alikiri hujisikia furaha kupambana na kumshinda bingwa kama Nadal.
Wawrinka hajawahi kushinda hata seti moja katika michezo yote 12 aliyokutana na Nadal huko nyuma, na alicheza fainal yake ya kwanza akiwa kwenye nafasi ya 19 ya ubora wa tenesi duniani.

No comments:

Post a Comment