Pages

Monday, January 6, 2014

SIMBA YAFUZU ROBO FAINALI BAADA YA KUIFUNGA KMKM 1-0

Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
SIMBA SC imefanikiwa kufuzu Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMKM usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kwa matokeo hayo, Simba SC inamaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi B, ikiwa na pointi saba, mabao mawili ya kufunga na haijafungwa, nyuma ya KCC ya Uganda yenye pointi saba pia, mabao sita ya kufunga na mawili ya kufungwa.
Wekundu wa Msimbazi; Kikosi cha Simba pamoja na makocha wao leo Amaan.

Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao hilo moja lilifungwa na Amri Ramadhani Kiemba kwa kichwa, akiunganisha krosi maridadi ya Ali Badru Ali dakika ya tano.
Kocha Mcroatia Zdravko Logarusic akiiongoza timu kwa mara ya kwanza kwenye mashindano haya tangu arejee kutoka mapumzikoni, alifanya mabadiliko makubwa katika kikosi cha kwanza leo, akiwapanga wachezaji wengi wa benchi.
Hata hivyo, wachezaji hao hawakumuangusha kwa kucheza vizuri na kama wangekuwa makini zaidi wangeweza kuondoka na mabao zaidi kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili, KMKM inayofundishwa na Ali Bushiri ilicharuka na kukaribia kufunga mara kadhaa, lakini hata hivyo bahati haikuwa yao na hadi kipyenga cha kuhitimisha mchezo kinapulizwa, walilala 1-0.
KMKM sasa inasubiri mustakabali wake wa kusonga mbele katika nafasi mbili maalum kwa makundi yote, kuungana na timu sita zitakazofozu moja kwa moja kutoka makundi hayo. 
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Yaw Berko, William Lucian ‘Gallas’, Omar Salum/Miraj Athumani, Gilbert Kaze, Donald Mosoti/Joseph Owino, Abdulhalim Humud, Uhuru Suleiman/Said Ndemla, Amri Kiemba, Betram Mombeki/Zahor Pazi, Ali Badru na Edward Chistopher/Adeyoum Saleh.
KMKM; Mudathir Khamis, Pandu Hajji, Haidhurun Juma, Khamis Ali, Iddi Kambi, Ibrahim Hatibu, Nassor Omar/Hajji Simba, Maulid Kapenta, Vincent Kamanya na Machano Abdallah.     

Mfungaji wa bao pekee la Simba SC katika mechi na KMKM usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Kombe la Mapinduzi, Amri Kiemba akimtoka beki wa wa wapinzani hao katika mchezo huo Mnyama alishinda 1-0 na kufuzu Robo Fainali ya michuano hiyo.
Zahor Pazi akiwalamba chenga mabeki wa KMKM
Abdulhalim Humud 'Gaucho' alicheza vyema katika kiungo
Beki wa KMM, Khamis Ali akimdhibiti mshambuliaji wa Simba SC, Ali Badru
Ali Badru akimtoka Khamis Ali
Miraj Athumani 'Madenge' akimtoka mchezaji wa KMKM
Kipa wa KMKM, Mudathir Khamis akidaka mpira mbeleya mshambuliaji wa Simba SC, Betram Mombeki huku beki wake akimlinda
Betram Mombeki akiutengeneza mpira mbele ya mabeki wa KMKM
Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola katikati akiwapa maelekezo ya kitaalamu wachezaji wake, Said Ndemla kulia na Adeyum Saleh kushoto kabla ya kuingia uwanjani wakitokea benchi
Kocha wa KMKM, Ali Bushiri akitafakari wakati mchezo ukiendelea huku timu yake iko nyuma kwa bao 1-0  

No comments:

Post a Comment