Pages

Sunday, January 5, 2014

AZAM YAFUZU ROBO FAINALI BAADA YA KUIFUNGA TUSKER 1-0

Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
MABINGWA watetezi, Azam FC wamefanikiwa kuwa timu ya kwanza kufuzu Robo Fainali za Kombe la Mapinduzi, baada ya usiku huu kuifunga Tusker ya Kenya bao 1-0, katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 
Hadi mapumziko, tayari Azam walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche baada ya kuchukua pasi ya Waziri Salum.
Mfungaji wa bao pekee la Azam leo, Kipre Tchetche akimtoka beki wa Tusker anayejaribu kulala kuokoa mpira
Wachezaji wa Azam wakimpongeza Kipre Tchetche kulia baada ya kufunga bao muhimu leo Amaan

Tusker ndiyo waliouanza mchezo huo kwa kasi na kupeleka mashambulizi langoni mwa Azam kwa takriban dakika 10, lakini baada ya hapo vijana wa Joseph Marius Omog wakazinduka na kuanza kuwapeleka Wakenya.
Safu ya kiungo ya timu ya Francis Kimanzi ilizidiwa mno na Azam na kutoa mwanya kwa wapinzani wake kuutawala mchezo.
Kpindi cha pili, Tusker walibadilika mno na kulishambulia kama nyuki lango la Azam, ingawa haikuwa bahati yao kupata bao.
Azam nayo iliyofanya mabadiliko ya safu yake ya ushambuliaji ikiwatoa Brian Umony na Joseph Kimwaga na kuwaingiza Muamad Ismael Kone na Seif Abdallah Karihe iliendelea kushambulia na kukosa mabao kadhaa ya wazi.      
Ushindi huo unaifanya Azam ifikishe pointi sita baada ya kucheza mehi mbili, wakati Tusker inabaki na pointi zake tatu. 
Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; Mwadini Ali, Erasto Nyoni/Malika Ndeule dk85, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Wilfred Michael Balou, Himid Mao Mkami/Jabir Aziz dk73, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Brian Umony/Muamad Kone dk57, Kipre Herman Tchetche na Joseph Kimwaga/Seif Abdallah dk70.  
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Anhtony Boki, Luke Ochieng, Martin Kiiza, Lloyd Wahome, Collins Okoth/Osborn Monday dk58, Andrew Tololwa, Dennis Nzomo/Frederick Onyango dk57, Jesse Were, Ismail Dunga na Michael Olonga/Ali Abando dk78.
 
Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche kulia akipiga mpira uliompita kipa wa Tusker FC ya Kenya, Samuel Odhiambo na kwenda nje sentimita chache kutoka langoni katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mapinduzi usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam FC ilishinda 1-0 na kuwa timu ya kwanza kufuzu Robo Fainali ya michuano hiyo.
Kiungo wa Tusker, Michael Olonga akiwatoka wachezaji wa Azam
Seif Abdallah wa Azam akimiliki mpira pembeni ya Martin Kiiza wa Tusker
Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam Fc akipasua katikati ya Uwanja
Beki wa Tusker akijaribu kumpokonya mpira mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche
Mshambuliaji wa Azam FC, Brina Umony akijaribu kuumiliki vyema mpira mrefu aliotanguliziwa
Kiungo mkabaji wa Azam FC, Kipre Balou akiondosha mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Tusker FC
Winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga akimuacha chini beki wa Tusker FC
Kikosi cha Tusker FC
Kikosi cha Azam FC

No comments:

Post a Comment