Pages

Monday, January 6, 2014

MANCHESTER UNITED 1 v SWANSEA CITY 2, BONY AWATUPA NJE UNITED KWENYE FA CUP!

Manchester United wakicheza Mechi hii kwao Old Trafford kuwakaribisha Swansea City kwenye FA CUP, United ndio walianza kufungwa mapema dakika ya 12 kupitia mchezaji Wayne Routledge baada ya kuwachomoka mabeki na kupaisha mpira hadi langoni mwa United, Dakika 6 baadae United wakasawazisha bao hilo kupitia mchezaji wao Javier Hernández baada ya mpira kupigwa kama kona na na hatimae Chicharito kumalizia mpira huo na kufanya matokeo kuwa 1-1.Dakika ya 90 Wilfried Bony akawamaliza United kwa kuwapiga bao la kichwa na kufanya mtanange kuwa 1-2 dhidi ya wenyeji United. Timu ambayo katika Historia yao haijawahi kushinda Old Trafford. Sasa Swansea City wanaendelea na raundi nyingine ya nne.
Kocha wa United David Moyes akisalimiana na mascot Fred the Red wa United muda mfupi kabla ya mechi kuanza.Midfielder Kagawa akipanga kuwachomoka wachezaji wa Swansea City leo kwenye FA CupDanny Welbeck Wayne Routledge wa Swansea City akishangilia bao lake kwa aina yake kimya kimyaKilio kwa United, baada ya kuanza wao kunyolewa!!Kipa wa United Anders Lindegaard nae Hoi!Antonio Valencia kwenye patashika akitaka kuwatoka wachezaji wa Swansea CityBaadae dakika ya 16 Chicharito  alisawazisha bao na hapa wakipongezanaChris Smalling  nae tena kwenye patashika

MATOKEO:
FA CUP: RAUNDI YA TATU
Jumapili Januari 5
Nottingham Forest 5 v West Ham 0
Sunderland 3 v Carlisle 1
Derby 0 v Chelsea 2
Liverpool 2 v Oldham 0
Port Vale 2 v Plymouth 2
Manchester United v 1 Swansea 2

No comments:

Post a Comment