Pages

Thursday, January 30, 2014

JOSE MOURINHO AWAKUBALI WEST HAM UNITED, WAMETUCHEZEA STAILI MPYA NA YA KARNE YA 19.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameponda aina ya uchezaji wa timu ya West Ham United na kudai kuwa ni wa karne ya 19 kufuatia timu yake kutoa sare ya bila ya kufungana katika Uwanja wa Stamford Bridge. Chelsea walifanya kila wanaloweza kuhakikisha wanapenya ngome ya West Ham wanaonolewa na Sam Allardyce lakini walishindwa na kujikuta wakigaana alama hivy kushindwa kuwafikia Arsenal ambao wameshuka mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Akihojiwa Mourinho amesema kuwa mchezo waliocheza West Ham wa kizamani na haufanani na timu iliyokuwa katika Ligi Kuu. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ni ngumu kucheza mechi wakati timu moja pekee ndio inayotaka kucheza huku nyingine ikifanya kazi ya kuzuia pekee.

No comments:

Post a Comment