Pages

Thursday, January 30, 2014

PEP GUARDIOLA AKUBALI TONI KROOS KWENDA OLD TRAFFORD, ANGALIA NA WENGINE WALIONUNULIWA NA TETESI

Dirisha la Uhamisho likifikia Siku yake ya mwisho leo Ijumaa Januari 31, huko Germany kuna habari kuwa huenda Kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos, huenda akatua Manchester United kufuatia kauli ya Meneja wa Mabingwa hao wa Germany, Pep Guardiola.

Akiwa bado amebakisha Miezi 18 kwenye Mkataba wake wa sasa na Bayern, Toni Kroos, Miaka 24, amekataa kuongeza Mkataba mpya akidai nyongeza kubwa ya Mshahara ambayo Klabu hiyo inagoma kumpa ili kukwepa kuibua malamiko ya Wachezaji wengine. 

Jana Mchezaji huyo alionyesha hasira za wazi Uwanjani pale alipovua Glovu zake na kuzitupa kwenye Benchi la Bayern wakati alipobadilishwa kwenye Mechi ya Bundesliga na Stuttgart huku Bayern iko nyuma Bao 1-0 lakini iliibuka Washinda Bao 2-1 baada Thiago Alcantara kufunga Bao tamu la ushindi katika Dakika ya 93.
Inaaminika anaweza kuihama hivi sasa Bayern Munich kwa Dau la kati ya Pauni Milioni 20 hadi 25 huku kukiwa na tetesi akiwa Old Trafford atalipwa Pauni 150,000 kwa Wiki ambazo Bayern inagoma kumlipa.

Na Meneja wa Bayern, Pep Guardiola, amekaririwa akisema: “Ni Mchezaji muhimu lakini kwenye Soka vitu huenda haraka. Leo yuko hapa, kesho ameondoka!” 


TAARABT KUTIMKIA AC MILAN KWA MARIO 
KLABU ya AC Milan ya Italia imetangaza kuwa Adel Taarabt tayari amewasili klabuni hapo kwa ajili ya kumalizia taratibu za uhamisho wake. Kiungo huyo wa klabu ya Queens Park Rangers ambaye msimu alikuwa akicheza kwa mkopo Fulham anatarajia kuhamia kwa vigogo hao wa soka nchini Italia. Nyota huyo wa kimataifa wa Morocco mwenye umri wa miaka 24 alitua katika Uwanja wa Ndege jijini Milan kwa ndege binafsi na uhamisho wake unatarajiwa kukamilika kabla ya muda wa mwisho wa usajili wa dirisha leo saa sita za usiku. Taarabt atakuwa mchezaji wa pili kutoka Ligi Kuu nchini Uingereza kutua Milan Januari hii baada ya Michael Essien kukamilisha usajili wake akitokea Chelsea.Michael Essien
Michael Essien


YOBO ATUA NORWICH KWA MKOPO
Norwich imemsaini Beki Veterani wa Nigeria, Joseph Yobo, kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu kutoka Klabu ya Uturuki Fenerbahce.Incoming: Norwich City have confirmed the loan signing of Fenerbahce defender Joseph Yobo
Habari hizi zimethibitishwa na Meneja wa Norwich, Chris Houghton, ambae amelazimika kusaka Mtu kuziba nafasi ya Majeruhi Michael Turner.Jopseph Yobo
Yobo, mwenye Miaka 33, alijiunga na Fenerbahce Mwaka 2010 akitokea Everton kwa Mkopo ambao baadae ulikuwa Uhamisho wa kudumu baada ya kuitumikia Everton tangu 2002.



CHELSEA YAKARIBIA KUMSAINI KURT ZOUMA TOKA ST ETIENNE
Chelsea ipo karibu kumsaini Kurt Zouma wa St Etienne ya France.
Beki huyo mwenye Miaka 19 anatarajiwa kusainiwa na Chelsea hii Leo na kubakishwa Klabu hiyo ya France kwa Mkopo.
Chelsea tayari imewasaini Nemanja Matic na Mohamed Salah kwenye Dirisha hili la Uhamisho.
-----***********************----


MAN CITY YAWATAKA WAWILI WA PORTO

Manchester City wapo hatua nzuri ya kuwanasa Wachezaji wawili wa FC Porto, Eliaquim Mangala na Fernando.Eliaquim MangalaEliaquim Mangala
Beki wa France, Mangala, Miaka 22, anathaminiwa Pauni Milioni 35 wakati Fernando, Raia wa Brazil mwenye Miaka 26, yupo chini ya hapo.
Ikiwa Wachezaji hao watatua Etihad, basi njia itakuwa nyeupe kwa Joleon Lescott kwenda West Ham United.Fernando



LEO IJUMAA SIKU YA MWISHO, SOKONI NANI ANAUZWA, NANI ANANUNULIWA?Julian Draxler: The €30million man?Welcome with open arms: Newcastle are in the chase for Clement Grenier Seal the deal? Yevhen Konoplyanka is Liverpool's chief targetDani Osvaldo: Is the Saints striker on his way to Juventus?Mirko Vucinic: is he Gunner join Arsenal?
Is Kurt Zouma heading to Chelsea?Lewis Holtby: Set to quit the Lane?Fernando Alexandre: Can West Ham doa cut price deal before the window shuts?Down and out? Inter are reportedly in for NaniKlaas Jan Huntelaar: Could he end up playing in England?Saber Khalifa (R): Set for Everton loan switch?Ross McCormack: Sunderland are keen on the Leeds strikerDani Osvaldo: Leaving for Monaco?Luke Shaw: Will Chelsea or Man United prise him away from SouthamptonEliaquim Mangala: In David Moyes' sightsJavier Hernandez: Monaco are keenSteven Defour: Will Fulham lose out?Davide Astori: Wanted to shore up the Southampton defence
Diego Costa: Heading to Chelsea?

No comments:

Post a Comment