Pages

Tuesday, December 17, 2013

FIFA CLUB WORLD CUP MOROCCO 2013: GUANGZHOU 1 vs BAYERN MUNICH 3, FRANCK RIBERY, MARIO MANDZUKIC NA GOTZE WAIPATIA USHINDI BAYERN.


MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich, jana Usiku wameyaanza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu kwa kwa kuwatandika mabingwa wa China na Asia, Guangzhou Evergrande bao 3-0.Bayern Munich walipata mabao mawili kipindi cha mwishoni cha dakika za kipindi cha kwanza, Bao la kwanza likifungwa na mchezaji wao matata Franck Ribery.
Dakika ya 40 dakika tano kabla ya mpira uende mapumziko Franck Ribery aliifungia timu yake bao kwa shuti kali kwa kumalizia mpira uliokuwa umegonga posti upande wa kushoto.
Dakika ya 44 Mario Mandzukic anaipachikia bao la pili kwa bao la kichwa timu yake Bayern Munich na kufikisha bao 2-0 dhidi ya Guangzhou Evergrande. Dakika ya 47 kipindi cha pili
Mario Gotze akaifungia tena Bayern Munich Bao la tatu nakufanya mabao kuwa 3-0. Guangzhou Evergrande wamepata bao lao la pekee kupitia mchezaji wao Lloyd Dyer katika dakika ya 77.


Nusu Fainali
17 Desemba 2013
MECHI 4: 22:30 Guangzhou Evergrande 1 v Bayern Munich 3
18 Desemba 2013
MECHI 6: 22:30 Raja Casablanca 3 v Atlético Mineiro [Stade de Marrakech, Marrakesh]
Mechi Mshindi wa 5
18 Desemba 2013
MECHI 5: 19:30 Al Ahly v Monterrey [Stade de Marrakech, Marrakesh]
Mechi Mshindi wa 3
21 Desemba 2013
MECHI 7: 17:30 Aliefungwa MECHI 4 v Aliefungwa MECHI 6 [Stade de Marrakech, Marrakesh]
Fainali
21 Desemba 2013
MECHI 8: 22:30 Mshindi MECHI 4 v Mshindi Mechi 6

No comments:

Post a Comment